Maendeleo Ya Kiswahili Katika Teknolojia Ya Habari Na Mawasiliano Essay

3114 Words13 Pages
MAENDELEO YA KISWAHILI KATIKA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA) Aritamba Malagira, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Ikisiri Teknolojia ya habari na mawasiliano imekuwa ikikua kila siku kutoka simu ya kukoroga hadi simu ya mkononi, matumizi ya wavuti na nyinginezo nyingi, kwa kweli ni hatua kubwa ya maendeleo katika teknolojia. Hivi sasa watu wanawasiliana ndani ya sekunde chache kwa umbali wa kutoka bara hadi bara kupitia wavuti. Katika hali kama hii lugha za ulimwengu nazo zimekuwa zikijitahidi kukabiliana na ukuaji huu wa teknolojia kwa kutafuta istilahi mpya ili kuelezea dhana mpya za kiteknolojia zinazoibuka. Katika harakati hizi, Kiswahili hakiko nyuma, istilahi mpya za Kiswahili zimekuwa zikiundwa ili kukidhi haja ya kuwasiliana kupitia Teknolojia ya habari na mawasiliano. Makala hii inalenga kuangalia hatua iliyofikiwa na Kiswahili katika tasnia ya teknolojia ya habari na mawasiliano ikiwa ni pamoja na kuchunguza istilahi za ki-TEHAMA zinazotumika. 1. Utangulizi Teknolojia ya habari na mawasiliano imekuwa kiungo muhimu sana katika maendeleo ya watu duniani. Watu wamekuwa wakitumia teknolojia hii katika kufanya mawasiliano muhimu, kufanya bishara na mambo mengine mengi yanayowanufaisha watu. Kompyuta/ Talakirishi ni moja ya kifaa kilicholeta mapinduzi katika TEHAMA kama asemavyo Katambi (2011) “Kompyuta ama Tarakilishi katika lugha ya Kiswahili ni kifaa ambacho kimebadilisha kabisa mfumo wa maisha ya binadamu katika miongo takribani sita iliyopita. Kutokana na kuwapo kifaa hiki dunia imejikuta katika maendeleo makubwa kabisa kuliko kipindi chochote kile katika historia ya 1 kuwapo kwake. Kifaa hiki kimeleta mabadiliko makubwa Sana katika maisha ya kawaida ya binadamu. Kifaa hiki kimesababisha mambo mengi kufanyika katika hali ambayo hakika isingewezekana au ambayo awali ingeonekana kama ya

More about Maendeleo Ya Kiswahili Katika Teknolojia Ya Habari Na Mawasiliano Essay

Open Document